WANAFASIHI

                                                                     YALIYOMO
  •  PENINA MUHANDO
  •  EBRAHIM HUSSEIN
  •  MWALIMU J. K. NYERERE
  • SAID AHMED MOHAMED
  • MOHAMED SAID ABDULLA                                                   
  • KALUTA AMRI ABEDI
  • M.S. KHATIB
           
   1.     PENINA MUHANDO


Penina Muhando alizaliwa tarehe 3 mwezi wa machi mwaka 1948, katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro nchini Tanzania. Alisoma katika shule mbalimbali za Tanzania na baadaye alijiunga na masomo ya elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea sanaa za maonesho. Baada ya kumaliza masomo aliajiriwa hapo hapo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo alifanya kazi ya kusomesha masomo ya Sanaa za maonyesho. Vile vile aliandika na kuigiza tamthiliya. Aidha mwandishi huyu baada ya kuolewa na Bwana Mlama alibadili jina na kuitwa Penina Mlama. Hata hivyo, katika kazi zake mbalimbali ameendelea kutumia jina la Penina Muhando.
Mwandishi huyu ambaye kwa sasa amerudi tena Chuo Kikuu cha Dar es salam kusomesha baada ya kuwa amepumzika kwa muda kutokana na kutingwa na majukumu ya ukurugenzi katika asasi zinazojishughulisha na masuala ya wanawake. Baadhi ya asasi hizo na mashirika hayo yasiyokuwa ya kiserikali aliyoyafanyia kazi ni Foundation for African Women Educationalist (FAWE), shirika lenye makao makuu jijini Nairobi, Kenya, na pia asasi isiyo ya kiserikali iitwayo CAMFED yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam, Tanzania. 
Penina Muhando ameandika kazi mbalimbali kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza zote zikiwa na mchango mkubwa kwenye fasihi andishi hususani kwenye utanzu wa tamthiliya. Baadhi ya kazi hizo ni;

1.      Hatia (EAPH 1972)
2.      Tambueni Haki Zetu (TPH 1973)
3.      Heshima yangu (EALB 1974)
4.      Pambo (Foundation Books 1975)
5.      Modern African Theatre with special Emphasis on East Africa (1975)
6.      Talaka Si Mke Wangu (EAPH 1976)
7.      Nguzo Mama (DUP 1982)
8.      Lina Ubani (DUP 1984)
9.      The Challenge to the African Writers Today (1990)
10.  The Popular Theatre In Africa (1991).

                     
                                 Penina Muhando na Sanaa (Thieta) ya Umma
Sanaa (thieta) ya Umma ni aina ya sanaa za maonyesho au maigizo yaliyofanywa moja kwa moja na wanajamii wa eneo fulani wakishirikiana na wataalamu wa sanaa kwa lengo la kuyaibua, kuyaeleza na kuyatolea suluhisho matatizo ya watu wa eneo husika.
Muhando (1991), katika kitabu chake kiitwacho Culture and Develeopnment: The popular Theatre Apprach in Africa, anaieleza vizuri dhana ya “Thieta ya Umma” au sanaa kwa maendeleo ya jamii. Mhando anaitaja miaka ya 1970 kama nyakati za mwanzo katika vuguvugu la “Theata ya Umma” kwa nchi nyingi za Afrika. Majaribio kadhaa yalifanyika yaliyokuwa na lengo la kuitambuliisha dhana hii ya Thieta ya Umma kwa wanajamii. Kwa mfano nchini Kenya dhana ya Thieta ya Umma ilijulikana sana kwa jina la “Thieta ya Ukombozi”. Maigizo mengi ya namna hii yalizungumzia sana harakati za ukombozi wa kifikra, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa kwa mwafrika dhidi ya utawala wa kikoloni, kwa sababu hii ya msingi Wakenya wengi walipenda kuiita aina hii ya sanaa ya maonyesho “Thieta ya Ukombozi”. Jaribio mojawapo lililokuwa mashuhuri sana ni lile lililofanyika katika kijiji cha Kamiriithu huko Limuru nchini Kenya. Hapo mwanzo maiigizo haya yalitumia lugha za asili kama Gikuyu ya nchini Kenya na baadaye maigizo haya yalileta athari kubwa ndani ya maigizo yaliyotumia lugha ya Kiswahili kwa mfano Thieta ya Umma ya Penina Muhando na wenzake ilitumia lugha ya Kiswahili lakini ilifuata mfumo sawa na ule wa maigizo ya Kamiriithu.
(Mulokozi 1996), anaendelea kufafanua dhana ya Thieta kwa Umma. Anasema:
                            “Ili kufanikisha lengo la Thieta kwa Umma kiukamilifu, ilibidi igizo liwe katika lugha inayozungumzwa na wananchi wenyewe, ambayo katika Kamiriithu ya Limuru nchini Kenya ni Gikuyu. Mfano Ngugi wa Thiong’o na tamthiliya yake ya Nitaolewa Nikipenda ambayo kwa mara ya kwanza iliandikwa kwa lugha ya Gikuyu na kujulikana kwajina la Ngaahika Ndeenda kueleza mbinu za sanaa za maonyesho za jadi zilizotumika. Baadhi ya mbinu hizo ni pamoja na nyimbo na ngoma, lugha iliyosanifiwa kulingana na mzingira, maudhui yanayoakisi maisha na matatizo ya watu wenyewe na yanayoendeleza maslahi yao, ushirikishwaji wa mtu yeyote, badala ya wataalamu tu, katika sanaa, matumizi ya ishara na mbinu nyingine za kijadi.”

Ushiriki wa Penina Muhando katika kueneza dhana hii ya Thieta ya Umma ulikuwa ni wa kiwango cha juu sana. Mwanamama huyu alijidhatiti na kukaza Kibwebwe ili kuhakikisha kuwa sanaa za maonyesho zinaleta mantiki na kunufaisha jamii. Mtaalamu huyu wa sanaa za maonyesho na wenzake ambao baadhi yao ni pamoja na Amandina Lihamba, E. Chambulikazi, G. Marengo na baadhi ya walimu na wanafunzi wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo na Chuo kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Sanaa za maonyesho walitumika ndani na nje ya nchi. Nchni Tanzania juhudi hizo zilifanyika katika maeneo kadhaa, baadhi ya maeneo hayo ni Bagamoyo Mjini (Pwani), Mkambalani (Morogoro), Malya (Mwanza) na Msoga (Pwani). Nje ya mipaka ya nchi Penina Muhando alishiriki pia katika uhamasishaji wa Thieta ya Umma, baadhi ya nchi hizo ni Zimbambwe, Kameruni na Bangladesh.
Mulokozi (1996) katika kitabu chake cha Fasihi ya Kiswahili, anasisiti kuwa japokuwa Thieta ya Umma haikuanzia Tanzania lakini juhudi kubwa za kuendeleza aina hii ya sanaa za maonyesho kwa lugha ya Kiswahili zilizofanikiwa zaidi ni zile za Penina Muhando na wenzake.

   Penina Muhando Mwasisi wa Mkakati wa TUSEME
Katika kuhakikisha kuwa sanaa za maonyesho zinaleta tija katika maisha ya wanajamii, mama Penina Mhando (ambaye katika maandiko yake mengi ya kitaaluma anatumia jina la Penina Mlama na katika kazi zake za kisanaa anatuma jina la Penina Mhando), alianzisha mkakati wa kuwafikia vijana hasa wasichana na kuwaelimisha juu ya haki na wajibu wao ndani ya jamii kwa njia ya sanaa za maonyesho. Katika mahojiano yaliyofanyika kati ya mwasisi huyu wa TUSEME na utafiti huu, Mama Muhando alieleza mengi juu ya mkakati huu uliokuwa maarufu sana kuanzia miaka ya 1990. Katika mahojiano haya Mama Mhando aliitaja hadhira yake kama chanzo cha msukumo uliomshawishi yeye kuanzisha mkakati huu, alisema mwitikio mkubwa wa hadhira yake katika tamthiliya ya Nguzo Mama ndio uliomshawishi kubuni mkakati huu. Vilevile katika mahojiano haya Mama Mhando alionyesha mapenzi yake ya dhati juu ya mkakati huu. Jambo hili liliibuka pale ambapo mtafiti alipomuuliza swali lililouliza kuwa “Kazi zako zipi unazozipenda? Na ni kwa nini”? Mama Mhando alisema kuwa kwa dhati ya moyo wake aliupenda mkakati wa TUSEME zaidi ya tamthiliya zake andishi. Alisisitiza kauli yake hii kwa kusema kuwa vijana wengi katika Dunia ya tatu wamekata tamaa, wengi hawajui hatima ya maisha yao ya mbele. Lakini mabadiliko yaliyoletwa na mkakati wa TUSEME waliyaona wazi wazi. Walipokuwa wanafanya aina hii ya sanaa ya maonyesho mbele ya vijana na watoto waliopo vijijini kabisa waliona badiliko la ghafla, badiliko hilo lilihashiriwa kwa kujitokeza tabasamu na uso wa kuchangamka mwishoni mwa maonyesho hayo. Hivyo alifurahi sana kuyaona mabadiliko haya wazi wazi. Kuhusu mbinu zilizotumika katika kuendeleza mkakati huu wa TUSEME Mama Mhando alisema kuwa mbinu zilizotumika katika kuendeleza Thieta kwa Umma ndizo zilitumika katika kuendeleza mkakati huu wa TUSEME. Katika mkakati huu Penina Mhando na wenzake walitembelea mashule, vyuo na maeneo ya makazi ya watu kwa lengo la kutoa elimu kwa njia ya sanaa ya maonesho. Baadaye wanafunzi kutoka shule mbalimbali walikuwa wakikutana kila mwaka mkoani Dar es salaam kwa lengo la kufanya sanaa za maonyesho kwa mtindo wa kushindana. Serikali ya Tanzania chini ya Wizara ya elimu na utamaduni iliamua kudhamini mkakati huu. Jambo la kusikisha ni kwamba mkakati huu unasuasua, mpaka sasa takribani muda wa miaka kumi mpango huu hauja fanyika kikamilifu.
                                                                        NA
                                                           MWL. MAJUMBENI 
                                                                 

2.     EBRAHIM HUSSEIN
Ebrahim N. Hussein alizaliwa Mkoani Lindi, kwenye Pwani ya Kusini ya Tanzania, mnamo mwaka 1943. Hussein anasadikiwa kuwa mwandishi wa maigizo anayeongoza Afrika ya Mashariki. Ni mwanashahada wa sanaa za maigizo, na mhadhiri aliyewahi kufundisha katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Pia Ebrahim Hussein ana shahada ya juu (doctorate) kutoka Chuo Kikuu cha Humboldt, Ujerumani. Alifundisha sanaa za maigizo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1975 hadi 1985 ambapo alistaafu mwaka 1988. Alishinda tuzo ya Umoja wa Waandishi wa Vitabu wa Tanzania (UWAVITA) kama mwandishi bora wa maigizo ya Kiswahili.
Hussein aliibuka na kazi zake mnamo miaka ya 1960, kwa michezo ya kuigiza ya Alikiona uliotolewa mwaka 1967 na Wakati Ukuta uliotolewa mwaka 1969. Hii ilikuwa michezo ya kuigiza ya kijamii, iliyokuwa na mada za migongano na mabadiliko. Kazi zake za baadaye katika mfumo huohuo zilikuwa Sokomomo ambao haujatolewa, na Kwenye Ukingo wa Thim iliyotolewa mwaka 1988. Mchezo mwingine ni Kinjekitile, uliotolewa mwaka 1969, ambao ni mchezo wa kuigiza unaohusiana na vita vya Maji Maji, ambao aliutafsiri kwenye lugha ya Kiingereza mwaka 1971. Pia mchezo wa Mashetani ambao ulitolewa mwaka 1971 ni moja kati ya kazi zake bora kabisa, mchezo huu unahusiana na migogoro katika jamii nchini Tanzania wakati wa awamu ya “Ujamaa”. Arusi, ni mchezo ambao unajadili Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar. Jogoo kijijini na Ngao ya Jadi, iliyotungwa mwaka 1976, nayo pia ilihusisha mada za mgongano katika jamii pamoja na harakati za kuleta ukombozi kwa baadhi ya mambo.
Hussein anaweza kufananishwa na mwandishi wa Nigeria na mshindi wa Tuzo ya Nobel, Wole Soyinka. Kama Soyinka, Hussein ni mwasisi wa sanaa ya maigizo ya kisasa ya Kimajaribio. Kazi zake kama zile za Soyinka, daima huwa zinadadisi zinachemsha akili na huwa zimetayarishwa kwa ustadi na ufundi mkubwa. Hata hivyo, Hussein hajulikani sana nje ya ulimwengu wa lugha ya Kiswahili. Lakini kama Soyinka, Hussein analenga katika masuala ya dunia nzima ya maisha na matatizo ya jamii ya Kitanzania katika hali halisi ya Afrika Mashariki.
Kwa jumla, Hussein ni mtunzi wa maigizo ambayo yanapenya na kugusa hisia na mawazo ya watu. Pamoja na kuwa baadhi ya michezo yake imetungwa kwa ustadi mkubwa na utumiaji mzuri wa fasihi simulizi ya Kiswahili, hususani maigizo, katika kiwango ambacho hakikutarajiwa lakini michezo hii inaeleweka na kuleta mantiki. Ebrahim Hussein na Shaaban Robert wamefanikiwa kuipatia nchi ya Tanzania, mahali pake maalum katika ramani ya dunia ya fasihi, (Zeze, 1999).
                                             
                                                                       NA
                                                          MWL. MAJUMBENI 
                                                                

    3. MWALIMU J. K. NYERERE
 

Samandito (2013) anasema, watu wanamfahamu Mwalimu J. K. Nyerere kama mwanasiasa na kiongozi maarufu wa enzi zake. Anafahamika pia kama mwalimu na mwanafalsafa maarufu aliyetetea haki na usawa wa watu wote bila kujali rangi, dini na hata kabila. Mwalimu J.K. Nyerere anafahamika kwa kuasisi Falsafa ya Elimu ya Watu Wazima iliyoonekana yenye manufaa makubwa na endelevu miongoni mwa jamii za kimataifa zilizojihusisha na shughuli za maendeleo. Mwalimu Nyerere kama binadamu wengine alikuwa nazo sifa nyingine kama vile Baba wa familia, baba wa watoto saba, babu wa wajukuu ambaye alipenda kucheza nao. Joseph Warioba (2009) anathibitisha haya, akisema:
“Mwalimu Nyerere alikuwa inadamu wa kawaida. Maisha na chakula chake vilikuwa vya kawaida kabisa. Jumapili moja nikiwa kijijini kwetu wakati wa likizo, mke wangu kwa kuwa yeye ni Mkatoliki, aliamua kwenda kusali katika kanisa la Butiama. Niliongozana naye. Baada ya ibada Mwalimu alitukaribisha kwa ajili ya kifungua kinywa ambapo alikuwa amewakaribisha pia wajukuu zake. Chakula kilikuwa cha kawaida na watoto walikuwa wakipiga kelele na kufanya fujo nyingi, wakimwaga chai na maziwa huku wakimwita babu yao kwa sauti wakitaka hiki na kile. Mtu anaweza kuona ni jinsi gani Mwalimu alifurahia kucheza na wajukuu kama mzee au babu mwingine wa kawaida” (Tafsiri yangu).
Pamoja na hayo, Mwalimu Nyerere alikuwa mtaalamu wa lugha ya Kiswahili. Akiwa mtaalamu wa lugha, Mwalimu J.K. Nyerere alitafsiri kazi za tamthiliya za William Shakespeare za Julias Kaizari na Mabepari wa Venisi kwa lugha ya Kiswahili. Pia aliandika mashairi mengi kwa lugha ya kiswahili. Kupitia mashairi hayo, alikuwa akijibizana na kujadiliana na washairi wenzake. Jambo la msingi tu ni kwamba, Mwalimu Nyerere alikuwa mshairi, mpenzi wa ushairi, mpenzi wa malumbano ya washairi na alipenda mashairi ya washairi wengine. Katika utangulizi wa Mashairi ya hekima na Malumbano ya Ushairi yaliyokusanywa na Mathias Mnyampala mwaka 1965, anaonesha jinsi alivyopenda ushairi na hasa mashairi ya washairi wakongwe. Barua yake kwa Mathias Mnyampala ya tarehe 14/08/1965 inaeleza jinsi alivyopenda malumbano ya washairi. Inasemekana pia kwamba, akiwa madarakani, na hisia zilipomshika kutaka kueleza jambo zito, alitumia mashairi.
Karsten Legere (1999) anasema kwamba Mwalimu Nyerere alitoa mfano bora kwa kutafsiri tamthiliya mbili za William Shakespeare katika lugha ya Kiswahili. Katika kuthibitisha hili anasema:
“Mwalimu anakumbukwa wakati wote kama mwandishi na mtaalamu wa tafsiri za vitabu vyenye hadhi kubwa duniani kama vile tamthiliya za mwandishi mashuhuri wa Kiingereza Shakespeare ambavyo ni Mabepari wa Venis na Julias Kaizari. Kwa kuongeza, kabla ya uhuru, Julius Kambarage Nyerere alikuwa akiandika mashairi ambayo yalijumuishwa katika kazi za washairi wengine kama vile Mathias Mnyampala au Abdul Kandoro”. (Tafsiri yangu).

Legere anaendelea kusema kuwa Mwalimu J. K. Nyerere alikuwa mwandishi wa makala nyingi katika lugha ya Kiswahili ambazo zilichapishwa katika Sauti ya TANU. Makala mojawapo ilimsababishia kulipishwa faini na watawala wa serikali ya kikoloni kwa sababu walijisikia kukosewa heshima.
Naye Laurent Magesa(2011) katika makala yake (The Hidden Face of Mwalimu Nyerere) anaeleza kwamba Mwalimu Nyerere alichapisha mashairi kwa lugha ya Kiswahili yenye kubeba maudhui mchanganyiko: ya kisiasa, kijamii na kiidili. Nyerere pia alitafsiri tamthiliya mbili za mwandishi mashuhuri wa Kiingereza, William Shakespeare zikiwa na ujumbe wa kijamii na kimaadili. Pia alitafsiri sehemu ya Biblia Takatifu Agano Jipya katika mtindo wa kishairi. Alikuwa na lengo la kutuonesha kwamba Kiswahili kama lugha inao uwezo kama lugha nyingine kutumika katika kuelezea ujumbe wa aina yoyote hata kama ni tata (Tafsiri yangu).
Wataalam wa fasihi ya Kiswahili wanakiri kuwa, Mwalimu Nyerere alikuwa ni mahiri si wa lugha ya Kiswahili tu, bali pia wa Lugha ya Kiingereza na Kizanaki, ambayo ni lugha yake mama na katika taaluma ya tafsiri. Mwalimu Nyerere pia alikuwa hodari wa fasihi simulizi. Mara nyingi hotuba zake zilisheheni vielelezo kutoka fasihi simulizi ya Kiswahili – visa na mikasa.  Tunaweza kukumbuka hadithi ya Kijiji kilichokumbwa na baa la njaa na wakamtuma kijana mmoja kwenda kutafuta chakula na asirudi. Pia simulizi ya mke wa Kaisari aliyekuwa mzinzi. Harith Ghassany (2010:259).



Legere (1999) ni miongoni mwa wanataaluma walioandika juu ya uanafasihi wa Mwalimu J. K. Nyerere. Amemwonesha Mwalimu Nyerere kuwa ametoa mchango mkubwa sana katika kukuza na kuinua lugha ya Kiswahili. Anaeleza kuwa mwalimu Nyerere alikuwa jasiri na alichukua hatua madhubuti za kukienzi na kukitukuza Kiswahili ili kiweze kutumika katika nyanja mbalimbali za kijamii na kitaaluma. Anaendelea kusema kwamba Mwalimu Nyerere alitoa mfano bora kwa kutafsiri tamthiliya mbili za William Shakespeare katika lugha ya Kiswahili. Katika kuthibitisha hili anasema:
“J. K. Nyerere ni mfano unaong’ara kwa ubunifu na mchango wake mkubwa katika kukuza na kuinua hadhi ya lugha ya kiswahili katika Tanzania. Akitambua upinzani na mtazamo hasi uliotamalaki nchini Tanzania, alikuwa jasiri na alichukua hatua madhubuti zilizokikuza Kiswahili katika nyanja mbalimbali za matumizi. Hivyo, mwalimu anakumbukwa wakati wote kama mwandishi na mtaalamu wa tafsiri za vitabu vyenye hadhi kubwa duniani kama vile tamthiliya za mwandishi mashuhuri wa Kiingereza Shakespeare ambavyo ni Mabepari wa Venis na Julias Kaizari. Kwa kuongeza, kabla ya uhuru, Julius Kambarage Nyerere aliendelea kuandika mashairi ambayo yalijumuishwa katika kazi za washairi wengine kama vile Mathias Mnyampala au Abdul Kandoro”.(tafsiri yangu).
Anaeleza pia kwamba, J. K. Nyerere alikuwa mwandishi wa makala nyingi katika lugha ya Kiswahili ambazo zilichapishwa katika Sauti ya TANU. Makala mojawapo ilimsababishia kulipishwa faini na watawala wa serikali ya kikoloni kwa sababu walijisikia kukosewa heshima. Aliandika pia makala nyingine iliyokuwa na kichwa kilichosomeka, Mali ya Taifa. Anaeleza pia kwamba Mwalimu Nyerere aliandika ushairi wa kidini ambao ni tafsiri ya Biblia Takatifu kutoka Agano Jipya.
Kassam (2000) anamwelezea Julius Nyerere kuwa ni mwasisi na Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, anayejulikana si tu miongoni mwa viongozi wa nchi wanaoheshimika duniani na wasemaji wa ukombozi na utu wa Waafrika, bali pia mwalimu na mwanafalsafa mashuhuri wa masuala ya elimu. Anaendelea kusema kuwa, kabla Nyerere hajajiunga na siasa alikuwa mwalimu, na ndiyo matokeo ya maandishi yake juu ya falsafa ya elimu na mahusiano baina ya uongozi wa kisiasa na kitaaluma nchini, anapendwa na kuheshimiwa na Watanzania wote na hivyo humwita kwa jina la mwalimu. Anaendelea kuelezea kuwa Julius Nyerere anasifika pia kwa falsafa yake ya elimu ya watu wazima iliyoonekana ya kufaa na endelevu miongoni mwa jamii za kimataifa za elimu ya watu wazima na taasisi zisizo za kiserikali zilizojihusisha na shughuli za maendeleo. Kutokana na malengo yake mazuri na kujitoa kwa ajili ya elimu ya watu wazima aliombwa kuwa mwasisi na Rais wa heshima wa halmashauri ya kimataifa ya elimu ya watu wazima mwaka 1973.
Naye Mwansoko (2000) anaeleza mchango wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika fasihi ya kiswahili. Anatueleza kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa mpenzi na shabiki mkubwa wa ushairi wa kiswahili na ndiyo sababu huenda ilimsukuma kutafsiri kazi za Shakespeare. Hivyo basi Mwansoko anasema:,
“Mwalimu Nyerere alitafsiri tamthiliya za Shakespeare Julias kaizari na Mabepari wa Venisi kwa sababu mbalimbali: kwanza ni kwa sababu tamthiliya za Shakespeare ni miongoni mwa maandiko bora Ulimwenguni. Sababu ya pili ni ushabiki wake wa ushairi, alivutwa kutafsiri tamthiliya za Shakespeare kwa vile ziliandikwa kwa mtindo wa mashairi guni, yaani yale yasiyo na vina. Japo mashairi guni yametofautiana sana na mashairi ya Kiswahili ya kawaida au ya kimapokeo, bado yalimpatia Mwalimu Nyerere burudiko la kutosha baada ya kuchoshwa na kazi zake za kawaida”.
Mwansoko anaendelea kueleza kuwa,
“Katika siku za mwisho za uhai wake, Mwalimu Nyerere alijishughulisha sana na kazi ya kutafsiri. Alitafsiri Biblia kwa ushairi na tayari vijitabu vinne vya tafsiri hiyo vimeshachapishwa. Aidha Mwalimu keshasawidi tafsiri ya Plato ya “The Republic” ambayo bado haijachapishwa. Mwalimu Nyerere ameshachapisha mashairi yake katika magazeti, vitabu vya washairi wenzake na hata kuchapisha tenzi zake binafsi, kama vile Utenzi wa Tanzania! Tanzania! (1993)”.
Malangwa (2005) anaelezea matatizo yanayowapata wataalamu wanaojishughulisha na kutafsiri kazi za fasihi kutoka lugha chanzi kwenda lugha nyingine. Ameeleza uwezo wa Mwalimu Nyerere katika taaluma ya tafsiri na matatizo yaliyojitokeza. Akishughulikia kazi ya tafsiri iliyofanywa na Mwalimu Nyerere ya Mabepari wa Venisi anasema:
“Matatizo yaliyompata mfasiri (Mwalimu Julius Kambarage Nyerere) ni yale ya kiisimu na kifasihi. Matatizo mengine ambayo yanaweza kufanyiwa utafiti ni tofauti za kiisimu baina ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza, tofauti za kijiografia baina ya jamii za watumiaji wa lugha hizi na tofauti za kisanaa baina ya lugha chanzi na lugha ya tafsiri”. (tafsiri yangu).

Rose Shayo (2010/11) anamwelezea Julius Kambarage Nyerere kama mjasilia mali wa kisiasa wa wakati wake. Anaeleza pia kuwa, alikuwa mpigania haki na usawa wa waafrika wote. Licha ya kupingwa na baadhi ya wasomi, Shayo anaeleza kuwa Mwalimu Nyerere aliendelea kuwathamini wasomi na mchango wao aliutegemea zaidi katika ujenzi wa taifa la Tanzania. Anaeleza pia kwamba, licha ya Nyerere kuwa mkristo Mkatoliki, hakuwa na ubaguzi wa kidini na wala hakupendelea upande wowote wa imani wakati wa uongozi wake. Katika kuthibitisha haya, Shayo anasema:
“Nyerere akiwa mfuasi mzuri wa dini ya kikristo kwa dhehebu la Katoliki, hakuonesha kuathiriwa na uumini wake kwa kupendelea dini fulani au dhehebu. Yeye alikuwa muumini mzuri wa dini yake, akiwa Dar es Salaam hakukosa kuhudhuria misa za masifu kila siku asubuhi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja asubuhi katika kanisa kuu la Mtakatifu Josefu. (Tafsiri yangu).
Nyerere, licha ya kuwa mkristu Mkatoliki, aliwalazimisha wasimamizi wa shule za misheni kudahili wanafunzi wa madhehebu na imani zote. Mwaka 1969, shule zote ambazo hazikuwa za serikali zilitaifishwa na kuwa za serikali, isipokuwa zile za seminari tu (The Guardian, September 28, 2006). Aliendelea kuwaambia viongozi wa dini kwamba kanisa lazima limhudumie mtu kiakili, kiroho na kimwili. Anasema: “Kanisa lazima liwahudumie watu nje ya mipaka ya kanisa”. Kwa mfano, shule, hospitali na taasisi zake za kibiashara zisifaidishe kanisa na wakristu tu, bali hata wasioamini.
Kutokana na imani na mapenzi yake kwa watu wake wa Tanzania, Mwalimu Nyerere alisikitika sana alipogundua kuwa anawaacha kwani aliona kifo chake kabla. Shayo anasema: “ Nyerere alikiona kifo chake kabla hakijatokea. Muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda kutibiwa ng’ambo, alijua kwamba hatarudi akiwa hai, na hivyo kama maneno ya buriani kwa watanzania aliahidi kuwaombea kama alivyonukuliwa akisema: “Najua sitapona toka ugonjwa huu. Nasikitika kuwaacha watanzania wangu. Najua watalia sana. Lakini mimi nitawaombea mbele ya Mungu”.
Shayo anataja pia kazi alizoandika Mwalimu Nyerere zikiwemo za kifalsafa na kifasihi pia. Baadhi ya kazi anazozitaja ni: Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (1993), Biblia iliyotafsiriwa kwa Kizanaki. Mwaka 1996 aliandika ushairi na nyimbo za kiroho zilizotokana na Enjili za Matayo, Marko, Luka, Yohana na Matendo ya Mitume. Pia alitafsiri tamthiliya za William Shakespeare ambazo ni Julias Kaizari na Mabepari wa Venis kwa lugha ya Kiswahili na zilichapwa na Oxford University Press mwaka 1969.
Magesa (2011) anaandika kwamba, “Juhudi za mwalimu Nyerere katika kukiendeleza Kiswahili kama chombo cha kujielezea na elimu nchini Tanzania, Afrika Mashariki na Ulimwenguni kote zinajulikana vema. Alichapisha mashairi kwa lugha ya kiswahili yenye kubeba maudhui mchanganyiko; ya kisiasa, kijamii na kiidili. Kama haitoshi kueleza uzuri na uwezo wa lugha kuelezea mawazo mbalimbali, Nyerere alitafsiri tamthiliya mbili za mwandishi mashuhuri wa Kiingereza, William Shakespeare zikiwa na ujumbe wa kijamii na kimaadili. Pia alitafsiri sehemu ya Biblia Takatifu Agano Jipya katika mtindo wa kishairi. Nini alitaka kutueleza katika haya yote? Jibu jepesi ni kwamba kiswahili kama lugha inao uwezo kama lugha nyingine kutumika katika kuelezea ujumbe wa aina yoyote hata kama ni tata (Tafsiri yangu).
Mtaalamu huyu anagusia tu kuwa, Mwalimu Nyerere aliandika mashairi kwa lugha ya Kiswahili yenye maudhui tofauti, bila kuweka bayana maudhui ya mashairi hayo na mchango wake katika fasihi ya Kiswahili. Hajaeleza pia kama kazi hizo za kifasihi za Mwalimu Nyerere ziko wapi na zina mchango gani katika maendeleo ya fasihi ya Kiswahili. 

                                                NA
                              MWL. MAJUMBENI 
                                      





4. SAID AHMED MOHAMED


Said Ahmed Mohammed alizaliwa pemba huko  Zanzibar, Mnamo tarehe 12 Desemba 1947. Haku bahatika kupata malezi ya baba na mama ipasavyo kwani wazazi wake walitengana akiwa mdogo sana. Hivyo alilelewa na mama zake wakuu (mama zake wakubwa), Bi.  Jokhana Bi Rukia. Alisoma shule ya msingi Wete Boys, Pemba baadaye alihamia Kiembe samaki, Unguja. Kisha akapelekwa skuli ya Darajani (shule yenye watoto wenye vipaji) Unguja baadaye akaendelea na masomo yake ya sekondari katika shule ya upili ya Gulioni ambapo zamani iliitwa “King George The VI”. Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea akiwa kidato cha pili. Baada ya kuhitimu masomo yake ya sekondari alijiunga na chuo cha ualimu cha Nkurumah TTC kilichopo mjini Zanzibar mwaka 1966, ilishindikana kujiunga na kidato cha tano na sita kwani wakati huo kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hayati Abeid Aman Karume alipiga marufuku masomo ya kidato cha tano na sita.

Baada ya kuhitimu chuo alifundisha shule ya msingi Kizimbani kwa wiki mbili tu, halafu akahitajika kwenda kufundisha shule ya sekondari Utaani,  kuanzia 1969 hadi 1974. Saidi Ahmed Mohamed alifundisha masomo ya biologia, hesabu, kemia na pia Kiswahili. Baadaye alibahatika kusoma katika skuli ya International Correspondence kiwango cha kidato cha tano na sita. Baada ya kujiunga na kidato cha tano na sita alipanga kujifunza masomo ya sayansi lakini palikosekana vifaa vya kufanya masomo ya utekelezaji wa kisayansi yaani (practical) na hivyo alichagua kufanya masomo ya kisanaa.

Mnamo mwaka 1976 Said Ahmed Mohammed alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusomea shahada ya kwanza katika elimu akijikita katika kusoma  Isimu na Fasihi ya Kiswahili, baada ya kufuzu katika shahada hiyo alirejea nyumbani Zanzibar na kuwa mwalimu mkuu wa shule za msingi na upili za Hamamni kwa miaka  mitatu. Na baadaye alirudi  Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kujisajili kusomea shahada ya uzamili yaani (MA), katika Isimu Telekezi . Alipokuwa  akisoma  Chuo Kikuu cha Dar es salaam kipawa chake kilimvutia mwalimu kutoka Ujerumani aliyefundisha Isimu Linganishi na ya kihistoria bwana Sigmund Bruner. Hapo ndipo alipopata fursa ya kuelekea Ujerumani kufanya shahada ya uzamifu  yaani  PhD, alijiunga na Chuo Kikuu cha Karl Marx Leipzig Ujerumani mwisho wa mwaka 1981 na kukamilisha shahada ya uzamifu mwaka 1985 na kutunukiwa shahada ya udaktari,  kipindi hicho alikuwa pamoja na familia yake.

Baada ya kumaliza shahada yake ya uzamifu huko Ujerumani aliteuliwa na raisi wa Zanzibar wakati huo mzee Idris Abdul Wakil, kuwa mkurugenzi wa pili wa Taasisi ya  Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI), ambayo baadaye ilikuwa  Chuo  Kikuu  cha  Zanzibar (SUZA), hivyo kurejea nyumbani Zanzibar kwa miaka miwili na baadaye akaondoka kwa sababu za kisiasa na fitina za watu ambao haku wafahamu, akaelekea Kenya mnamo mwaka 1987 na kuwa mwenyekiti wa kwanza wa idara ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Moi mjini Eldoret na baadaye  kufundisha  Kiswahili  katika  Chuo Kikuu cha Nairobi  hadi mwaka  1990.

Said  Ahmed  Mohammed  aliondoka  Kenya  kutokana na matatizo aliyokumbana  nayo Moi-Kenya. Tatizo kubwa ni mtoto wake ambaye alifanyiwa visa mbalimbali  kama vile kutafunwa meno na mtoto wa kikenya na suluhu ya kisa hicho haikuwa sahihi kwa mujibu wake. Sababu ya kisa hicho ni utundu wa watoto pamoja na kasumba ya utaifa ambayo iliwafanya kumuona ni mgeni na kuanza kumnyanyasa. Hivyo kwa kuwa hakupenda wanawe wateseke aliamua kuacha kazi kwani ilifikia hatua  watoto wake hawakutakiwa kupanda  gari ya  shule. Alipotoka  Nairobi alielekea  Japan katika Chuo Kikuu cha Osaka, idara ya lugha za kigeni na hapo ndipo alipopata uprofesa. Alipotoka Osaka ndipo akaenda Chuo Kikuu cha Bayreuth, Ujerumani na kufundisha tangia  mwaka 1997 mpaka 2012.

Said Ahmed  Mohammed  alipenda kusoma, kutunga mashairi  na hadithi  fupi, alipokuwa darasa la tano alitungama shairi yaliyotumiwa na walimu katika madarasa ya juu. Kazi yake ya mwanzoni utunzi wa shairi ambalo  liliitwa “Nimfuge Ndege Gani Ili Nipate  Salama” mwaka 1960. Shairi hili lilifungua mdahalo mkubwa kwa wapenzi wa fasihi na wana fasihi. Baada ya hapo alipata hamu kubwa ya kuendelea kuandika. Hivyo  aliandika  mashairi  na kupeleka redio ya  Zanzibar. Alipata  hamasa zaidi kutoka kwa walimu wake ambao  ni  Mohamed Abdallah, na Kindi Abubakary ambao  waliona  kipaji chake na kumsisitiza  aandike.

Said Ahmed Mohammed  aliwahi kushiriki  mashindano ya liyoanzishwa  na idara  ya  Kiswahili BBC. Mashndano hayo yalihusu uandishi wa hadithi fupi za  Kiswahili. Mara nyingi hadithi zake zilishinda lakini kati ya vitabu hivi viwili, hadithiya “Sadiki  Ukipenda” ndiyo iliyompa umaarufu, katika hadithi hii mtunzi alionesha  umakini wake katika  kutunga visa bunilizi  ambavyo vilielezea  maisha  halisi ya  kila siku katika  jamii.


Said Ahmed Mohammed alirithi kipawa  cha usanii  kutoka kwa mama yake mkubwa ambaye alikuwa nyakanga. Mama huyu alikuwa bingwa wa kuimba nyimbo za unyago. Pia alikuwa mtunzi mzuri wa mashairi, na alipenda sana  hadithi za fasihi  simulizi. Uandishi  wa  Said Ahmed Mohammed zaidi ya kurithi kutoka kwa mama yake mkubwa, ulitokana pia na mafunzo ya elimu ya dini ya  kiislam, aliyoipata  kutoka  madrassa.

Said Ahmed Mohammed alivutika na kuanza kusoma riwaya, riwaya ya mwanzo kuisoma ilikuwa ni riwaya ya  Kiu( 1972), ikifuatiwa  na Nyota ya Rehemu (1976),  zilizotungwa  na Mohamed  M.S.  Baada  ya kusoma riwaya ya Kiu  ndipo alipopata hamu na shauku ya kuandika riwaya.  Riwaya  yake ya mwanzo aliyoiandika ni Asali  Chungu ( 1977), ikifuatiwa na Utengano (1980), na Dunia Mti Mkavu ( 1980). Aliendelea na jitihada za uandishi hadi kuwa muandishi maarufu na kupata tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Vilevile amebobea katika ugawa ushairi ambapo ametunga diwani mbalimbali, zikiwemo za kisiasa, kiuchumi, mapenzi na utamaduni. Diwani hizo ni kwa lengo la kuibua maudhui aliyokusudia muandishi huyu kama waandishi wengine wa kazi za fasihi. Ametumia fani katika kazi zake za fasihi mojawapo ya mitindo aliyotumia ni uhalisia mazingaombwe katika kazi kama vile, “Babu alipofufuka, Kivuli  Kinaishi, Amezidi  na Sadiki  Ukipenda, pia alitumia bunilizi, utomeleaji na taswira katika  kazi zake nyingi. 

Said Ahmed Mohammed ametajwa kama muandishi mashuhuri zaidi Africa Mashariki na hata Afrika nzima akiwa ameweza kuandika riwaya, Tamthilia, Mashairi, kazi za watoto na hata vitabu vya shule na vyuo. Baadhi ya kazi zake zimetafsiriwa kwa lugha za  kigeni, pia kuna miswada ambayo imechapishwa hivi karibuni ya riwaya  ya  Nkama  dume, Mhanga  Nafsi yangu, na kitabu cha kusoma katika darasa la saba kiitwacho  Gharama ya Amani kinachozungumzia fujo za kisiasa zilizotokea Kenya. Mwandishi huyu ni miongoni mwa waandishi wa  riwa  ya za  kimapinduzi na  kifalsafa.

Familiayake;

Profesa Said Ahmed Mohammed ana mke mmoja anayeitwa Rahma, na watoto wawili msichana na  mvulana. Msichana  anaitwa Najima jina linalo maanisha nyota na ,wa kiume anaitwa Mahirna  neno  la  kiarabu  lenye maana ya  mwenye  ujuzi na wote  wamekamilisha  shahada  ya kwanza.

KAZI ZAKE;

Inasadikika ameandika zaidi ya vitabu hamsini na  tano (55), vifuatavyo ni baadhi ya vitabu alivyoandika, kuna vitabu vya:

USHAIRI

Sikate  Tamaa (1980) Longman Kenya Ltd.
Kina   cha  Maisha.
Jicho la  Ndani  (2001), Nairob:Longhorn  Publisher.

TAMTHILIYA

Pungwa (1988), Longman  Kenya  Ltd.
Kivuli  kinaishi  (1990), Oxford  University  Press .
Amezidi  (1995),  East African  Educational  Publishers.
KitumbuakimeingiaMchanga (2004)Nairob :Longhorn Publishers ltd

RIWAYA

Asali   Chungu( 1989), East   Afracan  Publishers.
Babu  Alipofufuka  (2001), JomoKenyatta   Foundation.
Utengano (1980),  Longhorn   Publishers.
Tata   za  Asumin i(1990), Longman  Kenya.
Dunia  Mti  Mkavu (1980), Longman   Kenya  Ltd.
Kiza  Katika Nuru (1988), Oxford  University  Press.
Dunia   Yao (2006), Nairob:Oxford  University  Press.

                                          NA
                             MWL. MAJUMBENI 


     5. MOHAMED SAID ABDULLA

Mohamed Said Abdulla alizaliwa mnamo mwaka 1918 katika mtaa wa Malindi Zanzibar. Alipelekwa chuoni ambako alijifunza kusoma Kurani. Mwaka 1928 alisoma masomo ya msingi katika shule ya serikali. Alifanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari mwaka 1938 katika shule ya serikali pia. Baada ya kuhitimu aliajiriwa kuwa ofisa wa afya ambako alifanya kazi hiyo mpaka mwaka 1958 wakati ajira yake ilipokatishwa. Baada ya kuachishwa kazi katika idara ya afya alifanikiwa kupata ajira nyingine katika gazeti la Mkulima kama mhariri. Alifanya kazi hiyo hadi mwaka 1968 pale alipoachishwa tena kazi ya uhariri katika gazeti hilo. Baada ya kuachishwa kazi hiyo alipata kazi ya utayarishaji kipindi cha redio kilichoitwa Sadiki Ukipenda katika Sauti ya Unguja. Katika uhai wake alioa na kupata watoto wanne.
Katika taaluma ya fasihi mchango wake unaonekana sana katika taaluma ya riwaya kwani aliandika na kuchapisha riwaya saba pamoja na hadithi fupi moja kama ifuatavyo;

Mzimu wa Watu wa Kale ,Kisima cha Giningi, Duniani kuna watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Waume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, Kosa la Bwana Msa, Mke Wangu ambayo ni hadithi fupi. Mohamed Said Abdulla alifariki mnamo mwaka 1992. 
                                               NA
                             MWL. MAJUMBENI 
                                     
          6. KALUTA AMRI ABEDI 
Sheikh Kaluta Amri Abedi alizaliwa Ujiji Kigoma mnamo mwaka 1924 Baba yake Kaluta Amri Abedi aliitwa Abedi bin Kaluta. Kaluta Amri Abedi Alikuwa ni mtoto wa pili wa kiume katika familia ya watoto kumi. Sheikh Kaluta Amri Abedi alipofika umri wa miaka 6 hivi alianza masomo ya Kurani mwaka 1930. Baada ya miaka mitatu ya masomo ya kurani  aliingia katika  shule ya masomo ya Kizungu. Baada ya kumaliza elimu ya awali mwaka 1937 alijiunga na Shule ya Sekondari Tabora.Baada ya masomo yake ya sekondari Sheikh Kaluta Amri Abed alikwenda kusomea ukarani wa posta Dar-es-salaam 1942—1943 .Kaluta Amri Abed alikwenda kusoma elimu ya dini Rabwah Pakistan ambako aliweza kufaulu vizuri na kuweza kutunukiwa shahada ya elimu ya dini (Teolojia).
Sheikh.Kaluta Amri Abedi alioa mke wake wa kwanza 1941 ambaye aliitwa Zamda bint Sudi ambaye alibahatika kuwa na mtoto mmoja aliye itwa Radhia kabla ya kumtaliki kutokana na upinzani mkubwa uliotokana na mgogoro wa tofauti za kidhehebu yaani Kaluta alipo hamia madhehebu la Ahamadiyya tofauti na mke ambaye alitoka katika familia yenye imani ya madhehebu ya sunni. Sheikh Kaluta Amri Abedi alioa mke mwingine mwaka 1956 ambaye aliitwa Amina bint Hamisi Mlenzi ambaye alibahatika kuzaa naye watoto sita na kufanya jumla  ya watoto saba.
Sheikh Kaluta katika maisha yake amekuwa mtumishi wa serikali kwa nyadhifa mbalimbali,kama: aliwahi kuwa Mbunge wa kigoma, aliwahi kuwa meya wa kwanza mwafrika wa jiji la kwanza Dar-es-salaam, aliwahi kuwa mkuu wa mkoa jimbo la Magharibi,aliwahi kuwa waziri wa sheria,mpaka mauti yanamkuta alikuwa waziri wa maendeleo na utamaduni.
Katika dini Sheikh Kaluta alikuwa  Sheikh na mbashiri katika imani ya kiislam ya Ahamadiyya  alijishughulisha na  kueneza dini pamoja na kutafsiri  kurani katika lugha ya Kiswahili na lugha za kizungu.
Sheikh Kaluta Amri Abedi alikuwa na kipaji cha usanii. Kipaji hiki cha usanii kilianza kuonekana alipofika umri wa miaka 13, aliweza kutunga na kuimba  mashairi kwa  sauti nzuri na pia aliweza kudhibiti kanuni za mizani. Aliweza kusoma mashairi ya lugha ya Kiingereza, Kiurdu, Kiarabu na kiajemi.
            Mchango wa Kaluta Amri Abedi kwenye lugha ya kiswahili
Katika  maandishi ya Mathias Eugen Mnyampala yanayotaja historia ya maisha ya:
Sheikh Kaluta Amri Abedi, Mwandishi Mathias Eugen Mnyampala amemtaja Kaluta kama mtu hodari wa kutumia Lugha ya Kiswahili katika fani ya kuimba Tajuwidi, Mashairi na Tenzi kwa mahadhi ya namna mbalimbaali za Maghani.  Hivyo Mnyampala anaweka bayana mchango mkubwa wa Sheikh Kaluta Amri Abedi kwenye Lugha ya Kiswahili kama ifuatavyo:
           Kaluta Amri Abedi akiwa na umri wa miaka sita
 Kaluta Amri Abedi alionyesha dhamira ya kupenda Lugha ya Kiswahili, alianza kupigania matumizi ya Lugha ya Kiswahili tangu akiwa na umri mdogo kati ya miaka sita, ambapo akiwa mwanafunzi wa masomo ya Kurani alionyesha kutoridhika kujifunza Kurani kwa Lugha ya Kiarabu tu hata akadiriki kumuuliza mwalimu wake Kwa nini tunasoma kama kasuku hatuelewi yaliyomo katika aya za kurani tukufu?  Kwa nini kurani haitafisiriwi katika Lugha ya Kiswahili.”  Hata waalimu wake walipomjibu juu ya maneno ya Kiarabu kuonyesha ukamilifu wa aya na madai ya Masheikh wake kwamba kurani ikitafsiriwa ingeharibiwa maana yake tofauti na zilivyoteremshwa na Mwenyezi Mungu, Kaluta Amri Abedi hakuridhika na majibu hayo aliendeleza jitihada za kudai matumizi ya Lugha ya Kiswahili zaidi kuliko lugha zingine. Mnyampala (Uk. 10)
  Kaluta Amri Abedi kama mshairi
Sheikh Kaluta Amri Abedi alitumia kipaji chake cha kuimba na kughani mashairi na tenzi kuenzi matumizi ya Lugha ya Kiswahili akizidisha maneno yenye utamu wa lugha ya Kiswahili, nahau za lugha ya kiswahili .  Hali amabayo ilifanya kuwa motisha kubwa kwa wasomaji wa mashairi yake kuijua lugha na kuithamini kwa utukufu wake. Sheikh Kaluta Amri Abedi alitumia kalamu kuweka mchango wake katika kukuza lugha ya kiswahili, aliandika maandishi yanayofafanua kanuni za utungaji wa mashairi ya kiswahili,katika kitabu chake alichokiita  SHERIA ZA KUTUNGA MASHAIRI NA DIWANI YA AMRI (1953) – Katika uandishi wake alihamasisha lugha ya kiswahili Tanzania na Afrika Mashariki kwa umahiri wake:Kaluta aliwahi kutunga mashairi mbalimbali kwa lugha ya kiswahili ambapo hata alipo andika kitabu cha mashairi chenye kueleza kanuni za kutunga mashairi washairi wengiwlikipokea kwashangwe kubwa na kumsifia Rejea Almasi ya Afrika (Uk 81) ” anaeleza hiki ni kitabu  ambacho kimesadia sana kwa wale wanao taka kujifunza utunzi wa mashairi. Ni kitabu ambacho kinatumika mashuleni na hakuna mshairi wa sasa aliyeandika juu ya ushairi katika karne ya ishirini ambaye hakulazimika kumnukuu”.
Kaluta akiwa na umri wa miaka 13 tu alipofiwa na baba yake aliandika ushairi wa kumwombolezea Rejerea katika Almasi ya Afrika (Uk 13-14): 
Mola mrehemu baba, babaaliyenizaa,
Mola ni wewe Tawaba, mghofiri dhambi pia,
Peponi mpe maaba,na vyeo mzidishia,
Dua nitakabalia, Mola mghofiri baba,
Baba mwingi wa huruma kwa wema alinilea,
Akanitia kusoma,dini na dunia pia,
Akanifunza ya wema,ya akhera na dunia,
Dua nitakabalia Mola mghofiri baba
Baba nina mkumbuka, vile nilivyo mjua
Mkarimu hana shaka,mwenye hadhi na sitawa,
Ni mtu alotukuka,vyeo akavipandia,
Dua nitakabalia,Mola mghofiri baba
Huu ni mfano tu wa kazi ya ushairi inayoweza kuonyesha uwezo wake katika fani ya uga wa mashairi tangu akiwa mtoto mwenye umri mdogo.
  Kaluta Amri Abedi kama karii
Kaluta Amri Abedi  kwasababu ya umahiri wake katika kujishughulisha na lugha ya kiswahili na uga wa ushairi alichaguliwa kuwa Karii wa mashairi ya kiswahili (yaani msomaji, mkosoaji na mwelekezaji wa matumizi na maandishi ya lugha ya kiswahili); akiwa Karii wa Ushairi” alipokuwa  Tabora aliandika makala zake kuhusu kiswahili akasema kwa kukitukuza kiswahili huku akigusia historia yake na kukimanya kwakwe alisema: “Kwa bahati  tu nilizaliwa katika mji  ambao lugha inayosemwa ni kiswahili na utoto wangu nikasoma karibu vitabu vyote vilivyopatikana na vilivyokuwa vimeandikwa kwa lugha ya kiswahili kisha muda wote wa maisha yangu nikalazimika kukitumia kiswahili kama chombo maalumu cha kufanyia kazi nilizoshughulika nazo za semi na maandiko, ikatokea nikaanza kujali sana maneno na  nguvu yaliyo nazo, ufasaha na jinsi ya kutoa wazo lilete athari inayotakiwa, ikawa ninapoandika najitahidi kuchungua sana maneno  kuyachagua na kuyapima na kutwaa yale tu niliyo fikiri yana nguvu za kutosha kuwasilisha maoni yangu. Mnyampala (Uk46)
Kaluta alikuwa msomaji wa vitabu vya kiswahili aliweza kusoma maandishi ya waandishi wa kiswahili na alikosoa na kutoa maoni yake ili kuhakikisha kiswahili kinatumiwa kwa usahihi wake, hivyo alitumia muda wake kufuatilia maandishi na kuyafanyia marekebisho makosa ya lugha ya kiswahili katika maandishi ya waandishi.  Hali hii ilitokana na upenzi wake mkubwa kwa lugha tukufu ya kiswahili.
  Kaluta Amri Abedi kama mwanaharakati 
Sheikh Kaluta Amri Abedi alichochea kasi  ya matumizi ya lugha ya kiswahili, kwa madhumuni ya kutukuza lugha ya kiswahili. Mwandishi Mathias Mnyampala amemfafanua Sheikh Kaluta Amri Abedi juu ya ushupavu wake katika kutetea Misingi Imara ya Lugha ya Kiswahili. Anasema “Alikuwa hodari wa Mijadala kwa namna zote, kwenye mashindano ya dini wakati akiwa yungali kiongozi wa dini, alipambana kwa hoja na jamaa wengine katika lugha ya kiswahili kwa hoja zilizokiuka alishinda katika mambo mbalimbali mororo ya kidunia,” Pia alishinda malumbano yaliyotokea baina yake na Dkt Lyndon Harris kutokana na mashairi ya Guni hasa yaliyo ndani ya kitabu cha kilicho tafsiriwa na Mwl. Julius K. Nyerere kilicho andikwa na Shakespeare kinachoitwa Julius Kaisari .Mnyampala (Uk. 46 – 47)
           Sheikh Kaluta Amri Abedi alisisitiza zaidi lugha ya kiswahili huku akionyesha umma kwamba kiswahili ni lugha pekee inayofaa kuwa ya Taifa na Serikali, alisisitiza kuwa lugha ya kiswahili inazungumzwa na watu wengi zaidi kwa saababu imesheheni maneno mengi ya kibantu na sarufi yake ni ya kibantu hata imekuwa rahisi zaidi wananchi kujua na kujifunza kuliko lugha za kigeni.
Kwa msisitizo mkubwa Sheikh Kaluta Amri Abedi kwa kubainisha uzuri wa lugha iliyotukuka, lugha ya kiswahili alifikia kuandika maandishi ya kulikejeli kundi la watu wanaofanya juhuhudi za kujifunza lugha ya Kiingereza, Kiarabu,na Kifaransa kwamba watazijua kwa kiasi tu, hata kundi la wanaodhaniwa wana kijua kiingereza hakika yake ni kuwa hawakijui vilivyo, wakisema wanakisema cha matata matata, wakiandika pia wanaandika cha matata matata, na vyovyote vile ambavyo kujulikana kwalugha za kigeni kwa watu wengi kutakuwa kuzijua lugha hizo juu juu tu Mnyampala (Uk48).
           Ukweli Sheikh Kaluta Amri Abedi alikuwa na mapenzi ya dhati kwa lugha ya kiswahili, hata kumbukumbu yake iliyosomwa kwenye mkutano tarehe 18/01/1962 yenye kichwa “HATIMA YA KISWAHILI” iliashiria jinsi Sheikh Kaluta anavyoshika kalamu kwa makini kuweka bayana mapenzi makini kwenye lugha nzuri na makini ya kiswahili akitia motisha kwa washairi wa lugha ya kiswahili pamoja na watumiaji wa lugha ya kiswahili kuenzi, kutukuza na kuweka nia njema ya ari thabiti ya kujifunza lugha iliyotukuka  lugha ya kiswahili.Mnyampala (Uk.47).
           Sheikh Kaluta Amri Abedi alitafsiri Kurani Tukufu kwa lugha ya Kiswahili Mnyampala (Uk14).
Alipokuwa Waziri wa Sheria alitafsiri  sheria kwa lugha ya Kiswahili, hali hii ilifanya shauku ya watu kujifunza sheria kwa lugha ya Kiswahili. Mnyampala (Uk. 60).
             Kaluta Amri Abedi kama mwenyekiti wa chama cha kiswahili Afrika mashariki
 
Sheikh Kaluta Amri Abedi alifunguliwa wigo mpana wa kuitukuza lugha na uzuri wake pale alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha  Washairi wa Kiswahili kwa Afrika Mashariki, katika kipindi hicho Sheikh Kaluta Amri Abedi alihamasisha matumizi ya kiswahili akielezea lugha ya Kiswahili kuwa ni tunu waliyopewa kuwaunganisha, katika kipindi hicho  alishauri kiswahili kutumiwa katika elimu ya awali, kati  na vyuo vikubwa.  Kwahiyo mchango wa Kaluta Amri Abedi ni mkubwa sana katika maendeleo na ukuaji wa lugha ya kiswahili na  unafaa kuigwa na Watanzania na wana Afrika Mashariki kwa upana wa mawazo yake katika kuienzi lugha yetu ya asili Kiswahili.
                  
                  Kaluta Amri Abedi akiwa mwanasiasa
Sheikh Kaluta Amri Abed akiwa katika nyanja za siasa alitumia uwanja wa siasa katika kufanya juhudi za kuhakikisha ustawi wa lugha ya kiswahili katika matumiz, Kaluta akiwa waziri wa sheria alipiginia kiswahili kitumiwe katika shughuri za bunge, na ulisisitiza kiswahili kitumiwe katika kutafsiri sheria kuweka urahisi kwa sheria kueleweka kwa watu wote wa Tanzania ambao Lugha ya kiswahili ni lugha rahisi na yenye kueleweka kwa urahisi, Sheikh Bakri Abedi Kaluta Katika Almasi ya Afrika ameelezea katika kitabu chake kuwa akiwa waziri wa utamaduni aliendelea kupigania heshima ya kiswahili .Mara kwa mara alisisitiza juu ya umuhimu wa kutumia kiswahili katika shule zetu kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu.Sheikh Kaluta Amri Abedi kuonesha uzalendo katika lugha ya kiswahili aloiwahi kuwaondoa watoto wake kutoka shule ya msingi Agha Khan ambayo leo inaitwa Muhimbili, na kuwahamishia shule ya msingi ya Mnazi mmoja iliyo kuwa ikifundisha kwa kiswahili hiyo ilitokana na alipogundua watoto wake hawawezi kusoma vitabu vya dini vilivyo andikwa kwa kiswahili, Katika  (Uk 209-210). Pia Sheikh Kaluta akiwa waziri wa Utamaduni na maendeleo ya jamii aliwahi kuwa mmoja ya watu waliopendekeza kuanzishwa kwa Taasisi ya uchunguzi wa kiswahili ili iwe Taasisi yenye kusimamia matumizi ya kiswahili, Kwa mchango wake katika shughuli zake kuienzi lugha ya kiswahili Taasisi ya Ukuzaji wa Kiswahili wliamua kumtunuku cheti cha kumbukumbu ya Jubeleiya TUKI ya miaka75 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930-2005.

   Sheikh Kaluta Amri Abedi ametoa mchango mkubwa katika lugha ya kiswahili akiwa katika nyazifa mbalimbali kama ilivyo oneshwa kuwa alikuwa mwanaharakati wa kiswahili, Mshairi ambapo alitunga mashairi kwa kiswahili na kuimba lakini pia alikuwa mwandishi wa kitabu cha kanuni za kutunga mashairi,alikuwa mwanasiasa aliyetumia mwanvuli wa siasa kuendeleza juhudi za kuitukuza lugha ya kiswahili na kuendelea kuipigania itumike katika shughuli za bunge na pia shule za msingi, sekondari na hata vyuo vikuu,aliwahi kuwa karii na hata mwenyekiti wa chama cha mashairi Afrika mashariki.Wakati wote huu Sheikh Kaluta Amri Abedi alishadadia kiswahili kupewa kipeombele zaidi katika matumizi Tanzania na Afrika mashariki yote.Kwa kweli Sheikh Kaluta Amri Abedi ametoa mchango mkubwa katika kukua kwa lugha ya kiswahili anafaa kuigwa na kuenziwa na Watanzania na Wana Afrika mashariki kwa jumla.
                                              NA
                                MWL. MAJUMBENI 
                                  

Maandiko Kuhusu Kazi za Muhammed S. Khatibu


Katika utanzu wa ushairi kuna orodha kubwa ya malenga wa Kiswahili ambao wamewezesha ushairi wa  Kiswahili kufikia hatua iliyofikiwa sasa. Miongoni mwa malenga hao ni Muhammed S. Khatib.

Kwa mujibu wa waandishi na watafiti mbambali (taz. mfano Williady na Luhwago, 2013; Mosha, 2012 na 2013; Mrekwa, 2013 na 2014; Kasiga, 2015), wanasema kuwa  Muhammed S. Khatib  ni nguzo mpya ya uandishi wa ushairi katika fani ya utunzi wa mashairi. Wanamtaja kama mwandishi wa mashairi ya kizazi kipya aliyeleta ladha inayovunja utofauti kati ya wanausasa na wanamapokeo. Kwa mfano, Williady na Mrekwa (2013:102) wanasema:
                                      “Ukiyasoma kwa umakini mashairi ya Muhammed S. Khatib hasa yale ya Wasakatonge utagundua kuwa mwandishi huyu amelete ushairi wa aina yake wenye kuchanganya ladha ya kimapokeo na hii yetu ya kisasa. Hivyo twaweza kusema haya ni mashairi yanayoweza kukubalika pande zote mbili….”. (Williady na luhwago 2013:102).


Mosha (2012 na 2013), anamuona Muhammed S. Khatib kama  mwandishi wa ushairi aliyefanikiwa zaidi katika miaka hii ya karibuni ukilinganisha na waandishi wengine. Anayataja maeneo yaliyomsukuma kusema usemi huu wa mafanikio. Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na matumizi ya hali ya juu ya taswira, picha na jazanda yaliyosanwa vizuri kiasi cha kumfikirisha msomaji. Mhakiki huyu anaendelea kwa kusema kuwa kadri msomaji anavyoendelea kuisogelea zaidi fani ya msanii huyu katika diwani zake ndivyo anavyozidi kupata ujumbe na utamu ya kiuumbaji uliofichwa kwa mtindo ambao haumchoshi msomaji.

Mrekwa  (2013)  wamegusia kipengele cha maudhui katika Diwani ya Wasakatonge na Fungate ya Uhuru. Anamtaja Khatib  kuwa ni mwandishi aliyejitokeza na kuandika mambo yanayohusu jamii na mabadiliko yake.Hata hivyo,hawajachambua wala  kuonesha ni dhamira zipi au mambo gani yanayohusu jamii anayoyazungumzia Muhammed S. Khatib katika maandiko yake. Hivyo basi, licha ya kutuachia maswali kuhusu mambo hayo anayoyajadili Khatib, pia wanatuachia kazi kubwa ya kuyachunguza na kuyatafiti kwa kina maandiko yake ili kuweza kuyagundua na kuyaweka wazi, jambo litakalokuwa msaada kwa wasomaji na wapenzi wa ushairi, hasa ushairi wa kimapokeo na wakisasa katika kuyaelewa vyema maudhui yaliyomo katika ushairi wake.

 Kasiga (2015)  amekigusia kipengele cha maudhui katika ushairi wa Muhammeid S. Khatib. Kasiga ameonesha dhamira ya umoja na mshikamano kama miongoni mwa dhamira zinazojadiliwa katika Fungate ya Uhuru. Kasiga anatumia shairi liitwalo “Unganeni”(uk.1), ambalolinasisitiza muungano kwa wafanyakazi wote katika kutetea maslahi yao. Katika shairi hilo ubeti ufuatao unasema hivi:
“Wafanyakazi wa Afrika, tuunganeni,
   Na wakulima kadhalika, tushikaneni,
   Makabwela mnaosumbuka, tukutaneni,
   Tujiandae kwa Mapambano, yalo Marefu,
           Ushindi ni wetu.."


Katika ubeti huu, mshairi anatoa wito kwa wafanyakazi wote, kuungana kwa lengo la mapambano, katika ubeti wa tano (5) wa shairi hili mwandishi anaeleza lengo la mapambano hayo ni kupinga dhuluma zote wanazofanyiwa wafanyakazi.

Khamis (2011:106) anaeleza kuwa Khatib anaeleza kuwa jagini huyu anaustadi wa hali ya juu katika kutunga mashairi yenye lugha ya mnato na ambayo yanaweza kuimbika. Anashadidia hoja hii kwakusema kuwa tofauti na watunzi wengine wa mashairi ya kisasa ambao wanatunga mashairi yasiyoweza kuimbika kwa urahisi lakini Khatib haijalishi mashairi yake ni yakisasa au yakimapokeo lakini yanaweza kuimbika kiurahisi zaidi, anatoa mfano wa mashairi ya kisasa na yenyekuimbika kirahisi ni pamoja na ‘Maendeleo ya Umma, Mjamzito, Ruya, Gorila, Pungo, Mkata, Nilinde na Nalitote’.Ubeti wa kwanza kwenye shairi la Nalitote, mwandishi anasema:

Nalitote, mbao tugawane,
Kwa vyovyote, isiwezekane,
Iwe pute, mali tugawane
                                             Nalitote.

Williady (2013: 24) anamzungumzia Khatib kama mshairi aliyefungamana sana na nasaba za kimapokeo. Anadai kuwa Khatib inaonekana wazi huyasana mashairi ya kisasa kwa lengo la kutafuta ushawishi katika pande zote za mgogoro wa ushairi lakini mwenyewe anajibainisha sana kama mwanamapokeo.  Mtaalamu huyu anachambua mashairi ya Muhammed S. Khatib yaliyoandikwa kwa kufuata kanuni zote za urari wa vina na mizani. Mwisho mtafiti huyu anachambua baadhi ya mashairi ya kimapokeo ya mwandishi huyu.

Mapunda (2010:81) anatueleza kwa jumla maudhui yanayopatikana katika kitabu Wasakatonge na Fungate ya Uhuru. Mapunda anayaeleza mawazo ya Khatib kwa jumla sana jambo ambalo linatuachia kazi kubwa katika kuyafikia malengo ya utafiti huu. Mapunda ananukuliwa akisema kuwa diwani hizi za Wasakatonge na Fungate ya Uhuru ambazo zina mashairi yaliyotungwa na Mwalimu Khatib zina mashairi maziyo yanaelezea matukio ya kawaida juu ya ndoa na matatizo yake, shabaha ya kuumbwa kwa binadamu, mawaidha ya dini na kupigania uhuru wa kweli au mapambano dhidi ua ukoloni mambo leo. Aidha, Mapunda hajaingia kwa undani katika kuyachambua maudhui aliyoyataja. Pia hajatueleza ni kwa namna gani maudhui hayo yanajitokeza katika “Wasakatonge na Fungate ya Uhuru”, hivyo kutuachia pengo kubwa la kimaarifa katika kuyasoma na kuyaelewa mashairi ya Muhammed S. Khatib.

Hata hivyo, waandishi na wahakiki wengi walioshughulikia maandiko mwalimu Muhammed S. Khatib hawajakishughulikia kabisa kipengele cha picha na taswira katika Diwani za Wasakatonge na Fungate ya UhuruAmri. Jambo hili ndilo lililoleta uchochezi na kusababisha kufanyika kwa utafiti huu ili kuweza kuziba pengo la maarifa lililopo katika kuyasoma na kuyachambua mashairi ya Muhammed S. Khatib. Vilevile mapitio ya maandiko yaliyopitiwa yameweza pia kulibainisha pengo la maarifa lililojibainisha wazi kwa kuonesha kutokufanywa kwa tafiti kumhusu mwandishi huyu nguli na muhimu katika uga wa Kiswahili na hasa Fasihi na taaluma ya ushairi kwa jumla.


 

No comments:

Post a Comment


created by
MJENGCOMPANY CONTACT: 0714166682or e-mail: mjengcompany@gmail.com